Monday, December 28, 2015

TBL YAMWAGA MAMILIONI MASHINDANO YA MITUMBWI MUSOMA

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imemwaga zawadi ya zaidi ya shilingi milioni10 kwa washindi mbalimbali mashindano ya mitumbwi kupitia bia ya Balimi ambapo timu zaidi ya 30 za wanaume na wanawake zilikuwa zikichuana kwenye ufukwe wa bwalo la polisi uliopo mjini Musoma na kuhudhuliwa na mashabiki wengi,walioshuhudia timu ya Benedictor Chamba kutoka bwai wakiibuka mabingwa kwa upande wa wanaume na kujinyakulia shilingi milioni 1 na laki 2 huku timu ya wanawake ya Elizabeth Marani kutoka Nyarusurya wakiwa mabingwa na kujinyakulia kitita cha milioni 1






Wanaume wakipambana na makasia

Maandalizi ya kuanza mashindano
Meneja mauzo wa TBL mkoa wa Mara,Polycalip Makunja akihesabu kuashiria kuanza mashindano
kazi imeanza
Ajali pia zilihusika lakini huduma ya uhokozi ilikuwepo
burudani ni sehemu ya kunogesha
majaji wakiwa kazini
Mgeni rasmi RPC wa mkoa wa Mara,Philip Kalangi(katikati)akiwa na meneja mauzo wa kanda,Changwe,(kulia)na meneja mauzo wa mkoa wa Mara,Poly,kushoto,waakifatilia mashindano.
Timu kutoka baruti wakishangilia kuingia tano bora laundi ya kwanza

washindi upande wa wanawake wakimaliza mashindano na kushangilia



mabingwa upande wa wanaume wakimaliza mashindano
nahodha wa timu ya wanaume akijipoza na maji baada ya kumaliza mashindano
wakati wa kutoa zawadi
kiongozi wa timu ya wanawake akikabidhiwa kikombe na milioni 1
picha ya pamoja na washindi wanawake
bingwa upande wa wanaume akikabidhiwa kikombe



Read more »

Monday, December 7, 2015

HIVI NDIVYO MGODI WA ACACIA ULIVYOWAPA BURUDANI WAKAZI WA NYAMONGO

KATIKA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI WANAOZUNGUKA MGODI WA ACACIA-NYAMONGO,UONGOZI WA MGODI HUO UMEKUWA UKIFANYA MAONYESHO YA UJASILIMALI YANAYOKWENDA SAMBAMBA NA MICHEZO YA KUJENGA MAHUSIANO IKIWEMO MIPIRA,RIADHA NA HATA MASHINDANO YA KULA NYAMA KILO MOJA KWA DAKIKA 3 KAMA AMBAVYO UNAONA KWENYE PICHA HAPO JUU AMBAPO MSHINDI ALIJISHINDIA MBUZI MNYAMA

 KIKOSI CHA TIMU YA MCHEZO WA PETE YA ACACIA AMBAYO ILIPOKEA KICHAPO CHA MABAO 16 KWA 6 KUTOKA KWA TIMU YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYANGOTO
 KABLA YA MCHEZO SALAMU ZILIHUSIKA
 HAPA NI KABLA YA FAINALI YA MPIRA WA MIGUU KATI YA TIMU YA ACACIA NA KEWANJA AMBAPO KATIKA FAINALI HIYO,ACACIA ILISHINDA KWA CHANGAMOTO YA MIKWAJU YA PENATI
 KIKOSI CHA ACACIA
 KIKOSI CHA KEWANJA
 SEHEMU YA ZAWADI ZILIZOTOLEWA KWA WASHINDI
 HAPA MCHEZO WA NETBALL UKIENDELEA
 MPIRA UKIELEKEA KIMIANI
 LICHA YA MVUA KUBWA ACACIA WALISHANGILIA USHINDI WAO KWA KUPIGA PU-SHAP KWENYE MAJI
 HAPA ILIKUWA NI MCHEZO BAINA YA VIONGOZI WA JAMII NA VIONGOZI WA MGODI AMBAPO VIONGOZI WA MGODI WALIFUNGWA 2-1 NA WASHINDI KUONDOKA NA MBUZI WAWILI NA KIKOMBE

 WACHEZAJI WA TIMU YA VIONGOZI WA MGODI NA TIMU YA VIONGOZI WA JAMII WAKITAFAKARI JAMBO
 MASHINDANO YA KULA NYAMA YAKIENDELEA


 HAPA WANASUBILIWA WANAWAKE WENYE UWEZO WA KULA MKATE NA SODA AMBAPO MSHINDI ALIPATIKANA NA KUONDOKA NA ZAWADI YA MBUZI
 MASHINDANO YAKIENDELEA
 MSHINDI ALIYEMALIZA MKATE NASODA AKIOMBA MKATE MWINGINE!
 WANANCHI WALIJITOKEZA KWA WINGI KUSHUHUDIA
 MENEJA WA MGODI,GARY CHAPMAN,AKIZUNGUMZA NA KUTOA AHADI YA KUENDELEA KUWA NA MAHUSIANO MAZURI BAINA YA MGODI NA WANANCHI
 MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA TARIME AKITOA NENO LA KUFUNGA MAONYESHO HAYO

 ZAWADI ZIKITOLEWA KWA WASHINDI

Read more »

KAMATI YA UTENDAJI MRPC YAKUTANA KUPANGA MIPANGO




KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mara(MRPC),imekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho ikiwemo kupanga mipango yakuleta ufanisi.

Akifungua kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi zake zilizopo jengo la bodi ya pamba manispaa ya Musoma,Mwenyekiti wa chama hicho,Jacob Mugini,alisema wakati uliopo sasa ni kupanga mikakati ambayo itakipeleka mbele chama hicho.


Alisema licha ya mipango ya kuweza kufanikisha maisha bora kwa waandishi kwa kuweka misukumo kwa wamiliki wa vyombo ya habari kulipa vizuri stahiki za waandishi,ipo mipango pia ya kuanzisha gazeti litakalokuwa likihusisha habari za mkoa wa Mara.


Katika kikao hic ho,Mwenyekiti huyo alisisitiza suala la wanachama kuzingatia taratibu za chama ikiwemo kulipa ada itakayowezesha kufanya mipango mizuri ya chama.

 

Read more »