Monday, December 7, 2015

KAMATI YA UTENDAJI MRPC YAKUTANA KUPANGA MIPANGO




KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mara(MRPC),imekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho ikiwemo kupanga mipango yakuleta ufanisi.

Akifungua kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi zake zilizopo jengo la bodi ya pamba manispaa ya Musoma,Mwenyekiti wa chama hicho,Jacob Mugini,alisema wakati uliopo sasa ni kupanga mikakati ambayo itakipeleka mbele chama hicho.


Alisema licha ya mipango ya kuweza kufanikisha maisha bora kwa waandishi kwa kuweka misukumo kwa wamiliki wa vyombo ya habari kulipa vizuri stahiki za waandishi,ipo mipango pia ya kuanzisha gazeti litakalokuwa likihusisha habari za mkoa wa Mara.


Katika kikao hic ho,Mwenyekiti huyo alisisitiza suala la wanachama kuzingatia taratibu za chama ikiwemo kulipa ada itakayowezesha kufanya mipango mizuri ya chama.

 

0 comments:

Post a Comment