Wednesday, November 28, 2012

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM WATEMBELEA CLUB YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM WAKIWA NA MENEJA WA TANRODS MARA EMANUEL KOROSO PAMOJA NA WANA HABARI WA MARA WALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE

BAADAE WALITEMBELEA KATIKA BEACH MAARUFU YA MALTIVILA

Na Shomari Binda
        Musoma,

Waandishi wa Habari kutoka Clabu ya Dar es salaam City Press Clabu (DCPC) wamepongeza utendaji wa kazi unaofanywa na uongozi wa clabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara (MRPC) kutokana na kila kiongozi kuwajibika katika majukumu yake yanayomkabili na kuacha kuingiliana katika utendaji wa kazi na kumthamini kila Mwanachama.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa (DCPC) Joseph Kainga kwa niaba ya Viongozi na Wanachama wa Clubu ya Wandishi wa Habari kutoka Jijini Dar es salaam ambao wapo Mkoani Mara katika ziara ya mafunzo ya namna ya utendaji wa kazi wa Clabu za Waandishi wa Habari zinavyoendeshwa.

Alisema kutoka na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa (MRPC) Emanuel Bwimbo wamependezwa na namna ambavyo kila kiongozi katika nafasi yake anawajibika kwa ufanisi bila kuingiliana na kumpa nafasi kila Mwanachama pale yanapotokea mafunzo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa na Muungano wa Clabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Kainga alisema ziara waliyoifanya imekuwa na mafanikio kwao kutokana na masuala mbalimbali waliyojifunza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo makumbusho ya Baba wa Taifa Mwitongo Wilayani Butiama na katika viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi.

Alidai Clabu ya (DCPC) kwa sasa ndio kama inaanza kutokana na kukumbwa na matatizo mbalimbali ya migogoro takribani miaka 6 hivyo jitihada zinafanywa ili kuirudisha na kusimama kama zilivyo clabu nyingine ambazo zimekuwa na ufanisi na uwajibikaji umekuwa ni wa wazi.

"Tumejifunza mambo mengi kutoka (MRPC) kwa muda wa siku tatu ambazo tumekaa hapa Mara na limekuwa ni somo kubwa kwetu yote tutaenda kuyafanyia kazi baada ya kufika Dar es salaam na tutamueleza kila Mwanachama kila kitu ambacho tumekipata katika ziara hii,"alisema Kainga.

Alisema wakiwa katika Makumbusho ya Butiama wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Madaraka Nyerere ambaye aliwaeleza mambo mengi kuhusiana na makumbusho hayo ambayo mwanzoni hawakuyajua vizuri lakini kupitia ziara hiyo wamepata kuyafahamu.

Kwa upande wake mmoja wa Wanachama wa (DCPC) ambaye yupo katika ziara hiyo anayeandikia Gazeti la MTANZANIA Arodia Pater alisema kwa yale waliyojifunza kutoka (MRPC) wanaamini yataleta mabadiliko makubwa katika kuimalisha clubu yao ambayo kwa sasa wana malengo ya kuiletea mabadiliko ya haraka.

Arodia ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa (DCPC) alisema amejifunza mengi namna (MRPC) wanavyofanya utaratibu mzuri katika udhibiti wa fedha ambapo uwazi unakuwepo na kila matumizi ya fedha yanayofanyika yanaingizwa katika vitabu na kila Mwanachama anao uhuru wa kuhoji katika Mkutano Mkuu wa clabu.

Wakiwa Mkoani Mara Waandishi wa Habari kutoka Jijini Dar es salaam walitembelea kiwanda cha Mara milk kinachotengeneza maziwa ya aina mbalimbali pamoja na maji ya kunywa,kiwanda cha samaki cha Musoma Fish pamoja na maeneo mbalimbali ya shughuli za kiuchumi.

Read more »

Tuesday, November 27, 2012

KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA AZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MKOANI MARA

MABANGO MBALIMBALI  YAKIPINGA UKATILI WA KIJINSIA


KABLA YA MAMBO YOTE ILIANZA MICHEZO AMBAO TIMU YA WANAWAKE YA KITASAKWA ILIIFUNGA RYAMISANGA BAO 1-0




BAADA YA MICHEZO KAMANDA MWAKYOMA ALIKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KINA MAMA WATAKA MABADILIKO


BAADA ALIFIKA BANDA LA POLISI KITENGO CHA DAWATI NA KUPATA MAELEZO KUTOKA KWA MRATIBU WA DAWATI

BLOGGER MASTER WA MARA PRESS CLUB SHOMARI BINDA KULIA AKIWA NA MTANGAZAJI WA VICTORIA FM AHMED NANDONDE KATIKA UZINDUZI HUO

IKAWA NI KUELEKEA ENEO LA MAZUNGUMZO NA WANANCHI


NI MUHIMU KUSAINI KITABU CHA WAGENI


MKURUGENZI NYARUGENDA NAYE ALISAINI KITABU CHA KIJIJI CHA KITASAKWA

DC WA BUTIAMA MAMA ANGELINA MABULA NANE ALITOA NENO KABLA YA MGENI RASMI

MKURUGENZI WA ABC FOUNDATION NYARUGENDA AKIBANJUKA HUKUAKICHANGIA UJENZI WA OFISI YA KIJIJI

DIWANI WA KATA YA BWIREGI MWANA MAMA NYAGHETI ADAM AKIAGANA NA KAMANDA MWAKYOMA BAADA YA UZINDUZI
Na Shomari Binda
        Butiama,


JUMLA ya matukio 201 ya ukatili wa Kijinsia yamelipotiwa katika Jeshi la Polisi Mkoani Mara kutokea  maeneo mbalimbali ya Mkoa huo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba Mwaka huu huku jamii ikitakiwa kubadilika na kukomesha matukio ya namna hiyo kuendelea kutokea katika Jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi Absalom Mwakyoma alipokuwa akifungua kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake iliyofanyika katika Kijiji cha Kitasakwa Kata ya Bwiregi Wilayani Butiama iliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABC Foundation Chini ya Ufadhiri wa Shirika la (WILDAF).

Alisema idadi hiyo imeongezeka tofauti na mwaka uliopita ambapo katika kipindi cha Mwaka jana matukio ya ukatili yaliyolipotiwa yalikuwa 148 huku watuhumiwa 51 walifikishwa Mahakamani na kati ya hao watuhumiwa 10 tayari wamekwisha hukumiwa na wanatumikia adhabu zao gerezani.

Alidai Mwanamke ni mtu ambaye anachangia kwa kiasi kikubwa katika Maendeleo ya Kijamii ikiwemo kuchangia shughuli za Kiuchumi katika Jamii pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza Elimu kwa Watoto kwa kuwa wao kwa asilimia kubwa ndio wanaokuwa nao karibu hivyo anastahili kuheshimiwa na kupewa haki stahili.

Kamanda Mwakyoma alieleza kuwa Binadamu wote ni sawa na wanastahili kutambuliwa na kuheshimiwa utu wao hivyo ni wazi kwamba watu wote hususani Wanawake ambao wamekuwa wakinyanyaswa kutokana na jinsia zao ni ukiukwaji wa katiba ya Nchi na misingi ya Haki za Binadamu pale wanapofanyiwa ukatili.
Alisema Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kwa kushirikiana na Asasi mbalimbali zinazopambana na masuala ya ukatili wa kijinsia watahakikisha mapambano ya kukomesha ukatili wa kijinsia Mkoani Mara yanakomeshwa hususani kwa Wanawake na Watoto wanaofanyiwa Ukeketaji.

“Nimeajiliwa kwa kufanya kazi na ntahakikisha nawashughulikia kwa mujibu wa Sheria wale wote ambao bado wanaendeleza matukio ya unyanyasaji kwa Wanawake na Watoto pale watakapobainika na sasa ni wajibu wa kila Mwananchi kubadilika na kuachana na masuala hayo.

“Lazima Mwanamke aheshimiwe na kila mmoja tusione ajabu leo kumuona Kamanda wa Polisi akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu kwa maana sasa tumeamua kwa dhati kushirikiana na jamii katika masuala yote likiwemo suala la kupinga na kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na ndio iliyopelekea Mwaka 2007 ukaanzishwa mtandao wa Polisi Wanawake na baadae Mwaka 2009 likaanzishwa dawati la jinsia la Wanawake na Watoto,”alisema Kamanda Mwakyoma.

Awali katika uzinduzi huo wa siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia,Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula aliwataka Wanawake kutokuogopa kutoa taarifa zinazohusiana na masuala ya ukatili wa Kijinsia ili kila mmoja anaye husika aweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria ili hatua dhidi yao ziweze kuchukuliwa.

Alisema inahitajika mikakati madhubuti zaidi kwa lengo la kuondoa masuala ya ukatili wa kijinsia kwani pamoja na kuwepo Sheria za kuzuia masuala ya ukatili bado kumekuwepo na matukio kama hayo na kuwa kikwazo katika Maendeleo ya Wanawake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ABC Foundation,Eustance Nyarugenda alilishukuru Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) Kupitia Shirika la Kivulini kwa  ufadhiri wa siku hizo 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na kuahidi kuendelea na mapambano dhidi ua ukatili hata baada ya kumalizika kwa siku hizo.   

Read more »

Thursday, August 30, 2012

Mafunzo Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Mara Kuhusu Online Journalism Yaonyesha Mafanikio

Mwanahabari George Marato akimsikiliza kwa makini Mkufunzi huku wanahabari wengine wakiendelea na mazoezi

Read more »

Mtoto Azaliwa Na Vichwa Viwili Mkoani Mara

mtoto azaliwa na vichwa viwili katika hospital ya DDH Bunda Mara mtoto huyu alikaa kwa saa moja ni kisha kufariki dunia kwa habari zaidi tembelea www.belensichina.blogspot.com

Read more »

Wanahabari Wa Musoma Wapata Mafunzo Ya Online Journalism

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza kwa makini Mkufunzi wa mafunzo hayo ndg Lukelo Mkami

Read more »