Thursday, March 31, 2016

Mkuu wa mkoa wa Mara atoa wiki 3 wanaomiliki siraha kuzisalimisha


 MKUU wa mkoa wa Mara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama,Magesa Mulongo,ametoa muda wa wiki 3 kwa wananchi  wote wanaomiliki siraha kinyume cha Sheria kuzisalimisha polisi au kwa kiongozi yoyote kuangazia ngazi ya Kijiji kabla ya oparesheni kali kuanza ya kuwasaka na kuwachukulia hatua watu wote wanaomiliki siraha hizo.

 Akizunguumza na wakuu wa wilaya,wakurugeinzi na wenyeviti wa Halimashauri za mkoa wa Mara,Mulongo alisema zoezi hilo litawahusu wanaomiliki kinyume cha Sheria na wale wanaomiliki kihalali ili kuangalia uhalali wao wa kumiliki siraha kwa kuwa wapo ambao wanazitumia kinyume na mkataba wa umiliki wa siraha uliokuwepo kabla ya kuanza kuimiliki.
 Mulongo alisema mkoa wa Mara kwa sasa lazima uangalieika kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na rasilimali zilizopo na sio kushughulikia matukio ya ujambazi unaotokana na matukio ya kutumia siraha.
 Mkuu wa mkoa wa Mara akiiagana na viongozi wa mbalimbali wa mkoa wa Mara wakiwemo wakuu wa wilaya mara baada ya kumaliza kikao chake kwenye ukumbi wa mikutano wa mkuu wa wilaya ya Bunda

Read more »

Thursday, March 17, 2016

MKUU WA MKOA WA MARA,MAGESA MULONGO, APOKELEWA KUANZA KAZI RASMI

MKUU  WA MKOA WA MARA,MAGESA MULONGO,AKIPOKELEWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA NGAZI ZA WILAYA NA HALAMASHAURI ZOTE ALIPOFIKA KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA MKUU WA MKOA KWAAJILI YA KUANZA KAZI RASMI BAADA YA KUTEULIWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,JOHN POMBE MAGUFULI

 RC'MULONGO AKISALIMIANA NA MWENYEKITI WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA RORYA
HAPA AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA BUNDA,JOSHUA MIRUMBE,KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA RORYA PAMOJA NA MKUU WA WILAYA BUTIAMA

 MKUU WA MKOA AKISALIAMIANA NA MKUU WA KIKOSI CHA JKT RWAMKOMA
 MKUU WA UHAMIAJI MKOA WA MARA NAE AKIJIANDAA KUTOA SALAMU KWA MKUU WA MKOA


 SALAMU KWA VIONGOZI MBALIMBALI

 HAPA AKISALIMIANA NA MMOJA WA WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA
 SALAMU ZINAENDELEA
 SALAMU NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA
 VIONGOZI WAKISUBILI KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA KWENYE UKUMBI WA UWEKEZAJI WA MKOA

 RC'MULONGO AKIZANGUMZA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA MKOA WA MARA AMBAPO MOJA YA MAMBO AMBAYO AMEYATILIA MKAZO NI SUALA LA ULINZI NA USALAMA NA KUKOMESHA MATUKIO YOTE YA KIUHALIFU AMBAYO YAMEKUWA YAKILIPOTIWA KUTOKEA MKOA WA MARA

Read more »

Thursday, March 10, 2016

MKUU WA MKOA WA MARA AZINDUA UNYUNYUZIAJI WA DAWA YA UKOKO KUUA MBU


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kapten mstafu, Aseri Msangi, amewataka wananchi kuondokana na imani potofu kuwa upulizwaji wa dawa ya ukoko majumbani mwao kwa ajili ya kinga dhidi ya Malaria huchangia kupoteza nguvu za kiume.


Msangi ameyasema hayo juzi wakati akizindua zoezi la unyunyiziaji wa dawa ya koko lililofanyika katika wilaya ya Butiama  ambapo zoezi hilo litafanyika katika wilaya za Butiama na Musoma vijijini kuanzia machi 9 hadi April 22 mwaka huu ambapo jumla ya majengo 47,577 kwa Wilaya ya Butiama na 31,824 kwa Musoma vijijini zinatarajia kupulizia dawa ya ukoka.

Amesema imani potofu zimekuwa zikichangia kwa kiwango kikubwa kuzorotesha zoezi  hilo na kuwataka wanannchi kutoamini hivyo badala yake wawe tayari kushirikiana na wahusika pindi watakapokuwa wakiwafikia katika kaya zao.

Msangi amesema ugonjwa wa malaria mkoani Mara umekuwa tishio kwa asilimia 25 kutokana na taarifa ya utafiti wa viashiria vya Malaria na Ukimwi ulioendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kudai juhudi zaidi zinapaswa zifanyike kati ya wananchi na taasisi mbalimbali ili kufikia kiwango cha kitaifa cha kupunguza malaria ambacho ni asilimia 9.

Hata hivyo amefafanua kuwa ugonjwa huo bado unaongoza kwa wagonjwa wengi wanaolazwa katika vituo vya afya na zahanati kwa nchi 10  za kusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania ambapo nchi hizo zimekuwa zikichangia  takiribani asilimia 70 kwa ukubwa wa ugonjwa huo duniani.


Amesema kutokana na utafiti ina maana kwamba mtu mmoja anapoteza maisha kwa kila dakika moja kutokana na ugonjwa huo na kwa mwaka 2012 iliua watoto takiribani 482,000 wa umri chini ya miaka mitano na kudai ni jukumu la kila mmoja kutokomeza ugonjwa huo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Abt Associates  la Marekani ambao wanasaidia kutokomeza Malaria nchini Tanzania na Afrika kwa Ujumla,Dk. Nduka Uwuchukwu, amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha ugonjwa huo unapungua na kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Amesema jukumu la kupambana na Malaria ni la kila mmoja na ni muhimu kuhakikisha kila kaya inanyunyuziwa dawa ya ukoko ili kuteketeza mazalia yote ya mbu waenezao Malaria katika wilaya za Butiama na Musoma vijijini.

 MKUU WA MKOA AKIPOKELEWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA VIWANJA VYA OFISI YA HALIMASHAURI YA BUTIAMA
 TIMU YA WANYUNYUZIAJI
 MKUU WA MKOA AKITETA JAMBO NA DK.NDUKA ANAYEONGOZA TIMU YA WANYUNYUZIAJI KAMA M KURUGENZI WA SHIRIKA LA Abt
 MKURUGENZI WA Abt AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI
 MKUU WA MKOA AKIELEKEA KUZINDUA
 AKIPATA MAELEKEZO KABLA YA UZINDUZI
 AKIJIANDAA KUZINDUA


 BAADAE MAELEKEZO YALITOLEWA NYUMBA ZOTE ZINYUNYUZIWE

Read more »

Wednesday, March 9, 2016

ILIVYOKUWA HARAMBEE YA MARA PRESS CLUB ILIYOENDESHWA NA DC WA TARIME


 
 JUMLA YA SHILINGI MILIONI 15 IKIWA NI FEDHA TASLIMU PAMOJA NA AHADI,ZILIKUSANYWA NA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA IKIWA NA LENGO LA KUFIKIA MILIONI 35 KWAAJILI YA KUANZISHA GAZETI LITAKALOWEZA KUUTANGAZA MKOA WA MARA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUWAVUTIA WAWEKEZAJI ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA MALTIVILA BEACH
 HAPA MWENYEKITI WA ZAMANI WA MARA PRESS CLUB,EMANUEL BWIMBO,AKIZUNGUMZA JAMBO WAKATI WA HARAMBEE HIYO
 MAKAMU MWENYEKITI WA MARA PRESS AMBAYE ALIKUWA MUONGOZAJI WA SHUGHULI HIYO
 MWAKILISHI WA GRUMENT FUND,ANGELINA MSECHU,AKIZUNGUMZA NA WALIOSHIRIKI HARAMBEE HIYO NA KUAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MARA PRESS BAADA YA KUWEZESHA KUFANYIKA KWA HARAMBEE HIYO

 MWENYEKITI WA MARA PRESS CLUB,MUGINI JACOB(KUSHOTO)AKITETA JAMBO NA MKUU WA WILAYA YA TARIME, GLORIOUS LUOGA,ALIYEKUWA MWENDESHAJI WA HARAMBEE HIYO
 WANACHAMA WA MARA PRESS WAKIFATILIA HARAMBEE HIYO
 BAADA YA SHUGHULI NZIMA UKAFUIKA WAKATI WA MAAKULI
 VILIVYOANDALIWA KWAAJILI YA KULIWA


 MISOSI ILIKUWA YA KUTOSHA

 MAAKULI INAENDELEA
 WAANDISHI WA MKOA WA MARA NA WADAU WAKIPATA CHAKULA


 BAADA YA CHAKULA NA MAMBO YOTE IKAWA NI KUAGANA KWAAJILI YA MAJUKUMU MENGINE

Read more »