Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi
wa Habari nchini Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo, akifungua Mkutano
Mkuu wa Wanachama wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of
Tanzania Press Club- UTPC) unaofanyika La Kairo Hotel Jijini Mwanza kwa
siku mbili kuanzia leo Oktoba 06,2016 na Oktoba 07,2016.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ya
"Viongozi Mustakabali wa Press Clubs Upo Mikononi Mwenu"unajadili
masuala mbalimbali ikiwemo Mpango Mkakati wa UTPC kwa mwaka 2016/20
uliofadhiliwa na Shirika la "The Swedish International Development
Cooperation Agency (SIDA)"
Viongozi
wa UTPC wakiwa kwenye mkutano huo ambapo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
UTPC, Abubakar Karsan, Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo, Makamu wa Rais
wa UTPC, Jane Mihanji na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili UTPC Abdallah
Mfaume
Wajumbe wa bodi, UTPC, wakiwa kwenye mkutano huo
Mwenyekiti
wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akiwa na wajumbe wengine
kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa
Habari nchini UTPC
Mwenyekiti
wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kushoto) akiwa na wajumbe wengine
kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa
Habari nchini UTPC
Wajumbe
mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu
za Waandishi wa Habari nchini UTPC.Kulia ni mwenyekiti wa Katavi Press
Club,Walter Mguluchuma
Mweka Hazina Mara Press Club akichangia jambo kwenye mkutano huo
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mwenyekiti
wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC,
Deogratius Nsokolo (kushoto) kwenye mkutano huo
Mwenyekiti
wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais
wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) kwenye mkutano huo
Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga, Kadama Malunde
(kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo (kushoto).
*****************************************
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuusoma na kuuelewa vyema mswada sheria ya huduma ya vyombo
vya habari 2016, uliowasilishwa na Serikali bungeni mjini Dodoma, kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya mswada huo.
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC Deo Nsokolo,
wenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano huo, unaofanyika kwa siku mbili Jijini Mwanza kuanzia leo.
Nsokolo amesema tayari kamati ya bunge
imekwisha kabidhiwa mswada huo kwa ajili ya kukusanya maon hivyo ni
vyema waandishi wa habari ambao wanaguswa moja kwa moja
na mswada huo, wakausoma kiundani na kisha kutoa maoni yao kabla ya kuwasilishwa bungeni ili kuidhinishwa.
Akiwasilisha
mswada huo katika bunge lililopita, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye, alisema ikiwa mswada huo utapitishwa na bunge
kuwa sheria,
utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya kitaaluma kwa wanahabari pamoja na huduma za vyombo vya habari nchini.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
SHUKRANI KWA GEORGE BINAGI WA BINAGI GROUP NA KADAMA MALUNDE WA MALUNDE 1 BLOG KWA PICHA NA TAARIFA KUTOKA KWENYE MKUTANO
Read more »